Kiwango cha vifo vya ugonjwa wa Monkey Pox kinapungua katika mkoa wa Kivu Kusini. Na hii ni kutokana na hatua ambazo idara ya afya ya mkoa imeweka kwa kutumia fedha zinazotolewa na UNICEF. Ubora wa huduma kwa wagonjwa umeimarika kulingana na msemaji wa kitengo cha afya cha mkoa. Daktari Claude BAHIZIRE anazungumza kuhusu hilo kwenye maikrofoni ya Jean Kasami.

Source: Radio Okapi